
Wakizungumza na EATV wavuvi hao wamesema kukosekana kwa vifaa vya uokoaii nako kumekuwa kukichangia wavuvi hao kuendelea kupotea baharini na kuziacha familia zao zikiteseka
Kwa upande wake mwenyekiti wa wavuvi katika soko la samaki Feri Ali Alawi amedai kwamba licha ya wavuvi hao kulipa fedha nyingi za leseni ya uvuvi na kodi mbalinbali lakini wamekuwa hawathaminiwi wanapooatwa na matatizo baharini kutokana na kuendelea kutumia mitumbwi na ngarawa katika kuvua samaki baharini
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa kikosi Cha majini ACP Moshi Sokolo amesema kazi ya uokoaji baharini inaenda sambamba na kuwaokoa wavuvi pale taarifa inapowafikia mapema