
Inaelezwa kuwa kwa sasa serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 470 kila mwaka kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi, lakini sababu kubwa inatajwa ni kutokana na kutokuwekwa kwa sera madhubuti za kuhakikisha mazao yanayozalisha mafuta ikiwemo alizeti yanapewa kipaombele.
Baadhi ya wakulima na wafanyabiashara wa alizeti mkoani Morogoro bado wanasema changamoto kubwa kwao ni kupata mbegu bora ambazo zitawasaidia kulima na kupata mavuno mengi ya zao hilo
Kutokana na hali hiyo wafanyakazi katika baadhi ya viwanda vidogo vya kukamua mafuta ya alizeti na wadau wa kilimo hiki mkoani Morogoro wanasema jitihada zinahitaji katika kilimo cha alizeti kufuatia wakulima kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya kilimo cha zao hilo