
Inaelezwa baada ya mauaji hayo aliuficha mwili wake katika stoo ya vifaa vya ujenzi katika nyumba ya Agatha Stanslaus
Polisi Kanda maalum Dar es salaam wameeleza kuwa Uchunguzi wa awali umeonesha mtuhumiwa huyo tarehe 06/07/2022 majira ya asubuhi alifika kwenye nyumba aliyokuwa anaishi binti huyo wa kazi akijifanya fundi wa umeme na kumueleza kuwa anataka kuweka balbu.
Inaelezwa kuwa alipoingia alimshambulia kwa kitu chenye ncha kali binti huyo na kumuua na kisha akavunja chumba cha mwenye nyumba na kuiba pesa Tsh 1,800,000/= na kutoweka.
Baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alikiri kumuua binti huyo, na Mwili wa marehemu aliuficha kwenye stoo ya nyumba hiyo huku akiwa ameufunika na vifaa mbalimbali vya ujenzi ili usionekane.
Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Jonas Ziganyige Mwenye umri wa miaka 71 mtaafu wa Jeshi la Wananchi, Mkazi wa Mbezi juu kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua Patient Romwadi 48 mfanyabiashara, Mkazi wa Wazo Mivumoni, Kinondoni.
Inaelezwa kuwa Marehemu akiambatana na Recy Renso (52) mkazi wa Posta walifika katika eneo hilo kwa lengo la kuangalia mipaka ya kiwanja chake ndipo mtuhumiwa alitoka ndani na kuonesha kutofurahishwa na kitendo cha watu hao ndipo alipoamua kuwafyatulia risasi na kukimbia ila baadae alikamatwa akiwa eneo la Kibaha Maili Moja akiwa amejificha.