Monday , 11th Jul , 2022

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Kenya Karanja Kibicho, amesema takriban maafisa wa Polisi 100,000 watatumika kulinda usalama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, mwaka huu. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani wa Kenya, Karanja Kibicho

Waziri Kibicho amesema nuchaguzi huo hautakuwa na fujo kwani maafisa hao watatumwa katika vituo vyote vya kupigia kura ili kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa bila matatizo.

"Tumejitayarisha kikamilifu kwa uchaguzi na hakutakuwa na fujo," amesema Dkt Kibicho.