
Rai hiyo imetolewa wakati wa mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika Wilaya ya Bariadi ukitokea Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, ambapo imeelezwa vijana na wanawake ndiyo makundi yanayoathirika zaidi na maambukizi ya ugonjwa huo wa Ukimwi.
"Baba, mama kaa na mtoto uzungumze naye. Mwelekeze mtoto nini cha kufanya juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, hususan watoto wa kike"
"Tunakumbushwa kuacha tabia hatarishi vinavyopelekea maambukizi ya virusi vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na ngono zembe"
"Pia ndugu zangu wana Bariadi, kupitia Mwenge wa Uhuru tunaendelea kukumbusha juu ya mapambano juu ya matumizi ya dawa za kulevya, chini ya kaulimbiu tunaelimishana juu ya dawa za kulevya kuokoa maisha," amesema Kiongozi wa Mbio za Mwenge.
"Pia, tumeupokea kwa furaha ujumbe wa Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 mwezi wa nane 2022, kwa kaulimbiu isemayo Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo, shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya Taifa. Sisi wana Bariadi tupo tayari kuhesabiwa," DC Kapange.
Katika hatua nyingi, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu 2022, amezindua mradi wa maji wa Sengerema Dutwa baada ya kuridhika na ujenzi wake na amewataka wakandarasi wanaojenga miradi yote ya maendeleo kuzingatia ubora halisi.
"Nanyi ndugu zangu, pindi mradi huu (wa maji) utakapokamilika na ninyi mvute maji majumbani kwenu. Mambo ya kutegemea DP (vituo vya kuchotea maji) siyo nzuri kwa sababu unaweza kumuta DP ipo kulee wewe unaishi hapo kutoka hapo mpaka kwenye DP ni shughuli tena," amesema Geraruma.
"Tunaishukuru sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwani toka alipoingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Sita takribani Bilioni 6,533,000 zimepokelewa kwa ajili ya kukamilisha miradi minane, ambayo imeongeza hali ya upatikanaji wa kutoka asilimia 58 Machi 2021, hadi kufikia mpaka asilimia 69.2 hivi sasa," amesema Injinia Mapengu.
"Lakini tukiamini kwamba wananchi wa mama Samia Suluhu Hassan (Rais) wataanza kutiririshiwa maji angalau kuanzia leo, wataanza kuoga, wtafua na wanafunzi wetu wataendelea kumeremeta na tutaendelea kufaulisha wanafunzi kwa sababu maji ni uhai," amesema Mbunge Kundo.