Thursday , 7th Jul , 2022

Benki ya CRDB inatarajia kutoa mafunzo ya biashara mtandaoni kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ambao wanafanya na wanaotaka kuanzisha biashara mtandaoni ambapo mafunzo hayo yatatolewa kupitia kampeni mpya iliyoanzishwa na benki hiyo ijulikanayo kama CRDB Instaprenyua.

Mkuu Wa kitengo cha Masoko kutoka CRDB, Joseline Kamuhanda

Akizungumza katika maonesho ya kimataifa ya biashara Sabasaba, Mkuu Wa kitengo cha Masoko kutoka CRDB, Joseline Kamuhanda, amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa tarehe 16 mwezi huu na yatashirikisha wadau mbalinbali wa masuala ya biashara wakiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA).