Baadhi ya washiriki wa mkutano huo
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar iko katika juhudi za kuhakiksiha inakuwa na madaktari bingwa wa fani mbalimbali wakiwemo wanaohusiana na maradhi ya mfumo wa utoaji wa haja ndogo katika kipindi kufupi kijacho.
Dr. Shein ametoa ahadi hiyo wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa wataalamu wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji haja ndogo kutoka Uingereza ambao kwa mwaka huu wameamua kufanya mkutano mkuu hapa zanzibar.
Mkutano huo unaofanyika mkoa wa Kusini Unguja ambapo Dk Shein amesema serikali yake imepania na ndio maana imewekeza zaidi katika vyuo vya afya na kuweka mitaaala maalum katika chuo kikuu cha Zanzibar lengo likiwa ni kupunguza hali ya sasa ambapo daktari mmoja anatibu watu 9700.
Naye Dkt Roger Plail akizungumza kwa niaba ya wataalamu wenzake amesema wataendeleza ushirikaino na madaktari wa Zanzibar ambao ndiyo uliowafanya waamue kufanya mkutano wao Zanzibar.
Katika mkutano huo ambao pia unahudhuriwa na wataalmu wa Zanzibar na Tanzania bara mada mbalimbali ziliweza kujadaliwa na wataaalmu hao..
Mmoja katika magonjwa ambayo hivi sasa yanaonekana kuzidi kwa kasi hapa nchini ni matattizo ya utoaji wa haja ndogo na kuwepo kwa mkutano huu ni moja ya mikakati ya seriklai kutafutia dawa tatizo hilo.