Romelu Lukaku akiitumikia Chelsea
Lukaku ambaye alisajiliwa kwa ada ya uhamisho ya Paundi Milioni 97.5 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi msimu uliopita,ameonekana kutaka kurejea Inter Milan ingawa maamuzi yapo chini ya mmiliki mpya wa The Blues Todd Boenhly.
Maamuzi ya Lukaku yanafuatia msuguano baina yake na Kocha ,Thomas Tuchel baada ya mshambuliaji huyo kuweka wazi kuwa hafurahii mbinu za mwalimu wake na angetamani kurejea Inter Milan.
Akizungumzia kuhusu usajili wa Lukaku, Mkurugenzi wa ufundi wa Inter Milan ,Giuseppe Marotta amesema hawana haraka juu ya kuinasa saini ya nyota huyo.
Nyota huyo ameshindwa kutamba na Chelsea ambayo ilimtarajia kutatua tatizo la kupachika mabao licha ya kumaliza msimu akiwa ndiye mfungaji bora wa Klabu akifunga mabao 15 katika mashindano yote.

