Wednesday , 1st Jun , 2022

Msanii Q Chief amemtaja Alikiba kama ndio msanii wake anayempenda wa muda wote kwa sababu hana mambo mengi na ameacha mziki wake uongee. 

Picha ya Q Chief kushoto na Alikiba kulia

Q Chief ameiambia eNewz ya East Africa TV kwamba 

"Ali its my favorite of all time kwa sababu hana makeke, hana mambo mengi, ameacha mziki wake uzungumze sana kuliko mambo mengine".

"Hii ndio sababu namuheshimu kila mara kutoka moyoni mwangu, kwanini nimkatae mtu  kwa sababu za tofauti za watu wengi".

Show ya eNewz ni kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 12:00 jioni.