Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji,
Hayo ameyasema katika maonyesho ya 9 ya biashara na utalii yanayofanyika jijini Tanga na kusema kuwa filamu ya The Royal Tour imeleta ushawishi kwa wawekezaji na watalii kuja nchini ambapo amewataka wafanyabiashara kujenga hoteli za kisasa na kutoa huduma zinazohitajika.
"Hoteli zote zimejaa kwa miezi mitatu ijayo hivyo nimewaambia umoja wa mahoteli hapa Tanga, mnaposikia majirani zenu wote hawana nafasi ya kuhudumia kilichobaki mbele yako ni wewe kujipanga vizuri na sasa ni Jiji la Tanga na mahoteli yake kupokea watalii na wawekezaji, "amesema Waziri Dkt. Kijaji.
