msanii Eddy Kanzo wa nchini Uganda
Staa huyu anayetamba kupitia ngoma yake ya 'Sitya Loss', ameweza kushiriki jukwaa moja na wasanii wakubwa Afrika, akiwepo Kenzo, Manni Bella, Tofan, Singuila na WizKid kati ya wengine, ikiwa ni moja ya maonesho yake makubwa kabisa kuwahi kufanya.
Star huyu anaweka rekodi ya kuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyeshiriki katika wimbo wa Hola Hola, ambao ni wimbo rasmi wa mashindano ya AFCON, nafasi ambayo ameitumia vizuri kupiga hatua nyingine katika upande wa muziki wake kimataifa.