Saturday , 17th Jan , 2015

Msanii na mtayarishaji filamu maarufu nchini, William Mtitu ametoa rai kwa wasanii na watayarishaji filamu nchini kujiendeleza zaidi kielimu katika tasnia hiyo, ili mwisho wa siku kuweza kuongeza ubora na mantiki katika kazi wanazozitengeneza.

William Mtitu

Mtitu ameiambia eNewz kuwa, kwa sasa tasnia ya filamu imekuwa kwa kiasi kikubwa kwa upande wa ubora na hata vifaa, ambapo amesema kuwa, itaongezeka maana zaidi endapo wale wanaotumia vifaa hivi watajifunza zaidi namna ya kufanya navyo kazi.

Mtitu amesema kuwa, kwa sasa filamu zinatengenezwa kwa kutumia vifaa vya kisasa kabisa huku kukiwa kuna nafuu ya kuviingiza nchini, na hivyo changamoto ya wataalam wa kutumia vifaa hivi ikionekana wazi.