Thursday , 21st Apr , 2022

Washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal imerejesha matumaini ya kumaliza kwenye nafasi 4 za juu kwenye ligi Kuu England EPL. Baada ya kushinda mabao 4-2 Ugenini dhidi ya Chelsea na kufikisha alama 57 sawa Tottenham walionafasi ya 4.

Arsenal wameinyuka Chelsea mabao 4-2 Stanford Bridge

Ushindi huu ni wa kwanza kwa Arsenal Baada ya kupoteza michezo mitatu ya Ligi mfululizo iliyopita dhidi ya Crystal Palace, Brighton & Hove Albion na Southampton na kupoteza matumaini ya kumaliza katika nafasi ya nne za juu kwenye Ligi itakayowapa nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Mabao ya ushindi ya The Gunners yamefungwa na Eddie Nketiah aliyefunga mara mbili, Emile Smith Rowe na Bakayo Saka. Mabao ya wenyeji Chelsea yamefungwa na Timo Werne na César Azpilicueta.

Hiki pia ni kipigo cha tatu kwa Chelsea mfululizo kwenye uwanja wao wa nyumbani Stanford Bridge. Baada ya kufungwa na Brentford mabao 4-1, Real Madrid mabao 3-1 na jana dhidi ya Arsenal 4-2, hivyo wamefungwa jumla ya mabao 11 kwenye michezo hiyo mitatu ya nyumbani.

Arsenal imesalia nafasi ya 5 ikiwa na alama 57 alama sawa na Tottenham walionafasi ya 4 waote wakiwa wamecheza michezo 32 na imesalia michezo 6 kabla ya kumaliza msimu.

 

Matokeo ya michezo mingine ya EPL iliyochezwa jana

Everton 1-1 Leicester City

Newcastle United 1-0 Crystal Palace

Manchester City 3-0 Brighton & Albion