
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 11:00 katika kijiji hicho baada ya bibi yao Tatu Moshi, kuwapiga kwa fimbo wajukuu zake wawili kisha kummwagia maji ya moto tumboni na miguuni mtoto mmoja na kusababisha kifo chake huku mwingine akijeruhiwa.