Wednesday , 13th Apr , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla amechukizwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Kusuasua kwenye usimamizi wa Miradi ya maendeleo hususani Zoezi la anuani za Makazi na Ujenzi wa Vituo vya Afya na shule yanayojengwa kupitia fedha za Tozo za Simu jambo lililosababisha miradi k

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Ilala, RC Makalla amesema hajaona sababu yoyote ya kuchelewa kwa miradi na zoezi la anuani za Makazi Kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Miundombinu yote wezeshi.

Kutokana Wilaya hiyo kutokuwa na mwanzo mzuri kwenye zoezi la anuani za Makazi, RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kupanga safu yake upya na kuhakikisha wanafanyia kazi dosari zilizojitokeza ili zoezi hilo liweze kukamilika.

Aidha RC Makalla ametembelea Ujenzi wa Kituo Cha Afya Segerea kinachogharimu Shilingi Milioni 250 na Kituo Cha Afya Kipunguni Milioni 250 ambapo amekerwa na miradi hiyo kuchelewa wakati Halmashauri nyingine zimesimamia vizuri Ujenzi na Sasa majengo yapo hatua za mwisho kukamilika lakini Ilala ndio kwanza wanajikongoja.

Hata hivyo RC Makalla amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Jumanne Shauri kubadilika huku akitaka Kitengo Cha Manunuzi nacho kujitafakari.

Hatua hiyo imekuja Baada ya Wataalamu kusema Ujenzi umechelewa Kutokana na msambazaji wa Vifaa vya Ujenzi (Supplier) Kusuasua kukabidhi Vifaa sababu ambayo RC Makalla amekataa kwakuwa ndani ya Wilaya hiyo Kuna viwanda vya kutosha vinavyozalisha Vifaa hivyo.

Pamoja na hayo RC Makalla ameshangazwa na Kitengo Cha Manunuzi kuwa na "kigugumizi" kushindwa kufanya maamuzi magumu kwa mzabuni wa kusambaza Vifaa licha ya kuona anakwamisha Ujenzi.