
Inaelezwa kuwa mke wake aligoma kumpakulia chakula hali iliyopelekea kumpiga ambapo naye alimvizia mumewe alipolala akachemsha uji na kummwagia usoni.
Mgeta anasema chanzo cha mkewe kufanya tukio hili huenda kimesababishwa na tabia yake ya kumpiga mara kwa mara anapogoma kumuandalia chakula.
Baadhi ya majirani wameeleza kusikitishwa na tukio hilo la kikatili lililohatarisha maisha ya kijana huyo.
Afisa mtendaji wa mtaa huo Bililiani Sabato amekiri kutokea tukio hilo kwenye mtaa wake huku akiwasii wananchi kuacha kujichukulia hatua mkononi inapotokea migogoro ya kifamilia badala yake watumie mamlaka kujipatia haki