
Wachezaji wa Biashara na Mbeya kwanza wakiwania mpira kwenye mchezo wa ligi Kuu uliochezwa Nyamagana
Bao la ushindi la biashara limefungwa na Deogratius Judika Mafie dakika ya 16 ya mchezo huo na sasa kikosi hicho kimepanda kutoka nafasi ya 14 hadi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi wakifikisha alama 22 baada ya ushindi wa Leo. Mbeya kwanza wao wamesalia nafasi ya 16 wakiwa na alama 14 na kipigo cha leo ni cha tatu katika michezo mitano ya mwisho.
Na hapo baadae utachezwa mchezo mmoja wa mwisho hii leo ambapo Azam FC watakuwa wenyeji wa vinara wa Ligi Yanga SC mchezo huu unachezwa Saa Saa 2 na 15 Usiku Uwanja wa Azam Complex