Wednesday , 6th Apr , 2022

Serikali ya Tanzania imesema katika kuendelea kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imedhamiria kuongeza idadi ya ndege zake na tayari imenunua ndege tano zaidi.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa katika hotuba yake ya bajeti Bungeni Jijini Dodoma amesema hadi Februari, 2022, Serikali imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege tano mpya. 

Amesema kati ya hizo, ndege moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner mbili ni aina ya Boeing 737-9; ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400, na ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F. 

Waziri Mkuu amesema lengo la serikali ni kuhakikisha (ATCL) inatoa huduma bora ya usafiri wa anga ndani na nje ya nchi.

Kukamilika kwa ununuzi wa ndege hizo, kutaiwezesha Tanzania kuwa na jumla ya ndege mpya 16.

Unaweza kutazama kauli ya Waziri Mkuu kupitia Youtube ya #EastAfricaTV