Tuesday , 5th Apr , 2022

Hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya inaanza rasmi usiku wa leo ambapo michezo miwili itapigwa majira ya saa 4 usiku. klabu ya benifica watakuwa wenyeji wa liverpool, mchezo utakao pigwa katika dimba la estadio da luz.

(Wachezaji wa Liverpool wakishangilia goli)

Kazi kubwa ya Benifica usiku wa leo itakuwa ni ya kuwazuia Liverpool walioshinda michezo yote 4 ya ugenini msimu huu kwenye michuano hiyo ya mabingwa barani ulaya. Pia Liverpool wanaingi akwenye mchezo huo wakiwa na rekodi ya kushinda michezo 16 kati ya 17 ya mwisho hadi sasa.

(Kocha wa Manchester City Pep Guardiola na Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone)

Na kule nchini England katika dimba la Etihadi matajiri wa jiji la manchester, Manchester City watawakaribisha Atletico Madrid ya Hispania, na ikiwa ni kwa mara ya kwanza timu hizi zinakutana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Naye kocha wa Atletico Madrid Diego Simeon amesema atayatumia maeneo dhaifu ya Manchester City kuweza kwadhiditi na kupata ushindi kwenye mchezo hu wa mkondo wa kwanza akiwa ugenini.

Michezo mingine ya robo fainaili ya ligi ya mabingwa ulaya itapigwa kesho ambapo klabu ya Chelsea itakua nyumbani darajani kuwakaribisha mabingwa wa kihistria wa michuano hiyo reala madrid, ambao kocha wake mkuu Carlo Ancelloti yuko mashakanRoaoi huenda akaukosa mchezo huo baada kukutwa maambukizi ya virusi vya corona. Na mchezo mwingine utakua kati ya Villareal dhidi ya Bayern Munchen.