
Droo ya hatua ya robo fainali klabu bingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika inafanyika kesho
Hatua ya makundi ya michuano hii ilikamilika jana kwa michezo ya mwisho ya hatua ya makundi kuchezwa kwenye makundi yote 4 na timu mbili za juu zilizomaliza nafasi ya kwanza na ya pili kwenye kila kundi ndizo zilizofuzu hatua ya robo fainali.
Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali upande wa klabu bingwa ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Club Athletic ya Morocco, Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia na Wydad Athletic Club ya Morocco hizi zimemaliza kama vinara wa makundi. Na zile zilizofuzu kama washindi wa pili kwenye makundi ni Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad, ES Setif zote za Algeria na Petro de Luanda ya Angola.
Kwenye kombe la shirikisho timu zilizofuzu kama vinara wa makundi ni Al-Ahli Sports Club ya Libya, TP Mazembe ya DR Congo, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na RS Berkane ya Morocco. Waliofuzu kama washindi wa pili ni Pyramids, al- ittihad, Al Masry na Simba sc.
Timu zilizomaliza kama vinara wa Makundi zitapangwa juu halafu zilizomaliza nafasi ya pili zitachaguliwa kucheza na vinara wa makundi katika droo ya kesho. Lakini pia vinara hao wa makundi watapata faida ya kuanzaia ugenini kwenye michezo ya mkondo wa kwanza na mchezo wa pili watamaliza katika viwanja vyao vya nyumbani.
Katika hauta hii timu zilizokuwa kundi moja haziwezi kukutana lakini zile zinazotoka kwenye nchi moja zinaweza kupangwa kucheza kwenye hatua hii.