
(Mkurugenzi mtendaji wa NBC Theobald Sabi na Rais wa TFF Wallace Karia wakisaini mkataba)
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi amesema bima hiyo maalumu itasaidia wachezaji na mabenchi ya ufundi ya vilabu huku ikiwa ni muendelezo wa uwekezaji mkubwa waliouweka kwenye ligi kuu Tanzania bara ambao ni zaidi ya shilling billion 9 kwa fedha za kitanzania .
"leo tunafuraha kutoa bima kwa zaidi ya wachezaji 640 wanaoshiriki kwenye ligi kuu sambamba na mabenchi ya ufundi na bima hii ni kwa ajili ya afya na maisha na hii bima itahusisha kwa hospitali za ndani na nje huku ikihusisha baba,mama na watoto wawili "amesema Sabi
Rais wa TFF Wallace Karia amesema wachezaji wanapaswa kufuata masharti ya mkataba sambamba elimu kuhusu bima iweze kutolewa zaidi ili kuweza kupata ufahamu zaidi wa juu ya bima na kuweza kulinda viwango vyao pindi wakiwepo uwanjani.
" tukio hili tunalolifanya linatuonesha jinsi gani ligi yetu ilivyo ya kulipwa (Proffesion),alafu unakuja kuona mchezaji wa ligi kuu anaonekana kwenye ndondo sio ya Shaffih pekee yake hata zingine sio kama hatutaki ndondo hapana tunazipenda na zina mchango lakini mchezaji akiumia je? ndio maana tunasema elimu itatolewa kwa wachezaji "amesema Karia
Bima hiyo ambayo haitajikita kwenye matukio ya nyuma yaliyotokea kwa wachezaji ingawaje nyota wa timu ya Polisi Tanzania Athanas Mdamu yeye atapata huduma maalumu kutoka NBC huku bima hiyo ikitolewa kwa kushirikiana na makampuni ya bima ya Sanlam na Britam