Monday , 28th Mar , 2022

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi amefariki Dunia pamoja na Dereva wake, asubuhi leo Machi 28, 2022 kwa ajali ya gari.

Kushoto ni marehemu Profesa Honest Ngowi aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na kulia ni gari alilokuwa anatumia lilivyoharibika baada ya ajali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chuo, ajali hiyo imetokea maeneo ya Pwani wakiwa njiani kutoka Dar es salaam kwenda Kampasi Kuu ya chuo hicho mkoani Morogoro.

Inaelezwa lori kubwa la mizigo lenye kontena liligongana na gari ndogo aina na Toyota Noah ambayo ikaligonga gari walilokuwa wanatumia Toyota Land Cruiser kisha ikaangukiwa na kontena na lori.

Tazama picha za ajali hapo chini