Monday , 14th Feb , 2022

Kocha wa Real Madrid Carlo Anceltti amesafiri na kikosi cha wachezaji 26 kuelekea nchini Ufaransa tayari kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya PSG, na kwenye kikosi hicho mshambuliaji Karim Benzema amejumuhishwa baada ya kukosa michezo 3 iliyopita.

wachezaji wa Madrid wakiwa kwenye ndege wakielekea Ufaransa

Benzema alifanya mazoezi jana Jumapili na amejumuhishwa kwenye kikosi cha wachezaji waliosafiri kwenda Jijini Paris Ufaransa, Benzema alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Januari 23 dhidi Elche.

Kurejea kwake ni habari njema kwa kocha Ancelotti kwani kwenye michezo mitatu aliyokosekana kikosi hicho kimefunga goli moja tu, Benzema msimu huu amefunga mabao 24 kwenye michuano yote msimu huu wa 2021-22.

PSG na Real Madrid wataumana kesho Jumanne kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya 16 bora utakaochezwa katika dimba la Parc des Princes majira ya Saa 5:00 usiku.

Hiki hapa kikosi kamili cha Real Madrid kilichosafiri kwenda ufaransa tayari kwa mchezo dhidi ya PSG

Magolikipa: Courtois, Lunin na Fuidias.
Mabeki: Carvajal, E. Militão, Alaba, Vallejo, Nacho, Marcelo naF. Mendy.
Viungo: Kroos, Modrić, Casemiro, Valverde, Lucas V., D. Ceballos, Isco naCamavinga.
Washambuliaji: Hazard, Benzema, Asensio, Jović, Bale, Vini Jr., Rodrygo na Mariano.