Mwanadada Sola Ogudugu wa Wizkid akiwa na Folarin a.k.a Falz kutoka nchini Nigeria
Hatua hii ya Sola, imeonekana kuchochewa na kitendo cha baba mtoto wake star wa muziki Wizkid, kuonesha dhahiri kumtenga na kutoka na wasichana wengine huku muziki ukiendelea kutengeneza daraja kubwa kabisa kati yao.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kutoka kwa Wizkid na timu yake kufuatia hatua hii ya Sola kuonesha kuwa hisia za kimapenzi kati ya wawili hawa zimekwishakufa siku nyingi licha ya kuendelea kuunganishwa na mtoto waliyenaye.