Thursday , 1st Jan , 2015

Katika kuingia mwaka  mpya wa 2015 ambao pia ni mwaka wa uchaguzi,viongozi wa dini wamewaasa watanzania kuchagua viongozi wenye sifa kwani mustakabali wa taifa uko mikononi mwa wananchi na sio vinginevyo.

Baadhi ya waumini katika ibada ya mwaka mpya, 2015

Akizungumza kwenye mahubiri ya ibada ya mwaka mpya katika kanisa la Mtakatifu Patrice, jimbo katoliki la Morogoro, paroko wa parokia ya kanisa hilo Padre Prochecy Kasongo, amewaasa watanzania kutumia mwaka huu wa uchaguzi kuchagua viongozi watakaoona wanafaa bila ushawishi.

Padre Kasongo pia amewataka watanzania kupigia kura katiba inayopendekezwa, huku waumini hao wakitakiwa pia kujipanga upya kiroho ili kuishi kwa amani na upendo katika mwaka huu.

Katika hatua nyingine watanzània wameaswa kuutumia mwaka mpya wa 2015 kujipanga vyema kwa ujenzi wa taifa, kuacha maovu na matendo mengine yasiyompendeza mwenyezi mungu, na kutowafanyia wengine yale tusiyopenda kufanyiwa.