Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko
Mboneka ameeleza kuwa ni kweli kumekuwa na changamoto ya wanafunzi wa kike waliofika katika umri wa hedhi kutofika shuleni kwa kukosa taulo za kike hivyo ameishukuru East Africa TV, East Africa Radio pamoja na Flaviana Matata Foundation.
Aidha Jasinta Mboneko amesema kuna fursa kubwa ya watu kuwekeza wilayani humo hususani kwenye sekta ya uchimbaji madini hivyo anawakaribisha wawekezaji wengi wa ndani ambapo pia ujenzi wa uwanja wa ndege ukikamilika kutakuwa na fursa nyingi zaidi kwenye viwanda.
Wafanyakazi wa East Africa TV na East Africa Radio wakiwa na mkuu wa Wilaya ya Shinya Jasinta Mboneko (katikati)
''Huko nyuma tulikuwa na tatizo kubwa sana ila tumekuwa tukiwaelekeza walimu wakuu na wakuu wa shule kuhakikisha kila mwezi mara mbili mara tatu kuzungumza na watoto wa kike kuhusu hedhi salama na namna ya kujitunza na hii imechangia mimba za utotoni kupungua,'' ameeleza DC Jasinta.
Wafanyakazi wa East Africa TV na East Africa Radio wakiwa na mkuu wa Wilaya ya Shinya Jasinta Mboneko (katikati)
Ameongeza kuwa, ''hizi taulo za kike zimekuwa zikisaidia watoto wa kike kutokosa masomo katika wilaya yetu maana unakuta mtoto anakosa masomo takribani siku 5 kwa mwezi sasa ukipiga hesabu ni siku nyingi sana na anakosa vipindi vingi sana''.