
Magari yanayotumia gesi asilia (NGVs) imesaidia kuboresha hali ya hewa, kuokoa gharama karibu zaidi ya nusu ya ile ya mafuta ya petroli, kupungua uzalishaji wa gesi chafu, kelele, harufu kidogo na kuleta unafuu katika sekta ya usafirishaji.
Takwimu zinaonyesha kuwa magari zaidi ya milioni 11 duniani yanatumia gesi asilia na nchi inayoongoza ni Pakistan yenye magari milioni 2.1, Argentina magari milioni 1.8 na Brazil magari milioni 1.7.