Monday , 9th Aug , 2021

Msanii Beka Flavour amefunguka stori za kuibiwa mpenzi wake Happy Reuter na msanii wa filamu Patrick Kanumba kwa kusema stori hiyo haijamuumiza na ameona ni vitu vya kawaida.

Kulia ni Beka Flavour kushoto ni Patrick Kanumba na Happy Reuter

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Beka Flavour anasema stori hizo ni za uzushi ujinga na hana mpango nazo.

"Hizo nimezichukulia poa tu hazijawahi kuniumiza, nimeona ni vitu vya kawaida sana hivyo vitu vipo na kila siku vinatokea, kuhusu story za baby mama wangu tuziache kwa sasa" amesema Beka Flavour

Kwenye mahusiano yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Aaryan Beka flavour.

Zaidi tazama hapa kwenye video.