Sunday , 8th Aug , 2021

Wakulima nchini wametakiwa kuachanana kilimo cha mazoea na kufanya kilimo biashara hasa katika kuongeza tija ya uzalishaji ili kukabiliana na changamoto wakati bei inaposhuka pamoja na kuweka kumbukumbu na kuwasiliana na wanunuzi kabla ya kulima mazao yao.

Pichani wakulima wakiwa shambani.

Kilimo cha biashara kinafanywa na watu binafsi, kampuni mbalimbali na taasisi zilizojipambanua kwa ajili hiyo ikiwemo Jatu iliyofanya uwekezaji ya kilimo cha mazao mbalimbali kwa ajili ya biashara.

Haya yanajiri katika mkutano mkuu wa wakulima wa JATU ambao una wachama 30,000 na wateja wanaokadiriwa kufikia 70,000 nchi nzima kwa sasa, wengi wao wakiwa vijana walioajiriwa na kujiajiri katika taasisi mbalimbali.

Jatu imewekeza katika mikoa mbalimbali nchini na tayari taasisi hiyo imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) na malengo yake kwa kipindi cha mwaka huu ni kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 7.5 zitakazoisaidia kuongeza tija katika kilimo ikiwemo ununuzi wa zana mbalimbali ,

Aidha kupitia mashamba kampuni ya JATU wamekuwa wakizalisha takribani tani 8,670 za nafaka ambazo huchakatwa katika viwanda vidogo vidogo walivyoanzisha katika maeneo ya Mbingu Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma