Thursday , 5th Aug , 2021

Watoto watatu wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakazi wa Kijiji cha Ngoile wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, wamefariki dunia baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na kundi la Simba huku mwenzao mmoja akijeruhiwa walipokuwa porini kutafuta mifugo yao iliyokuwa imepotea.

Kamanda wea Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 5, 2021, na Kamanda wea Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo, na kusema kwamba tukio hilo limetokea Agosti 3 mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku na watoto wote hao ni wanafunzi wa shule ya msingi Ngoile.

Tazama video hapa chini