Wednesday , 4th Aug , 2021

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu watano kwa madai ya kuiba na kufanyia uhalifu bastola yenye risasi 11 katika eneo la Forest Jijini Mbeya, ambapo jeshi hilo lilikuja kubaini kwamba bastola hiyo ni mali ya Mkuu wa wilaya ya Sikonge, John Palingo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ulrich Matei, akionesha bastola ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 4, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoani humo Ulrich Matei, ambapo hata hivyo hakueleza mazingira yaliyosababisha bastola hiyo ya Mkuu wa wilaya kukutwa ikiwa mikononi mwa wahalifu.

Kamanda Matei amewataja watu waliokamatwa na bastola hiyo kuwa ni Isaka William (24), Farew Raphael (30), Malodi Joseph (24), Daniel Kamwela (24) na Shadrack Msemwa (35) wote wakazi wa Iyunga Jijini Mbeya.