Sunday , 1st Aug , 2021

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amesema Serikali inaendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi kwa wakati pamoja na kutekeleza ahadi zake mbalimbali ikiwemo malipo ya madiwani.

Kikao cha Madiwani Halmashauri ya Kinondoni

Msigwa amesema hayo leo Agosti 1, 2021 mbele ya wanahabari ambapo ameeleza,  ''Wafanyakazi wote wa serikali wanalipwa mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi, hivi navyozungumza tayari mishahara wa mwezi Julai wameshalipwa. Jumla ya Shilingi Bilioni 630 zimelipwa tarehe 23.'' 

Ameongeza kuwa, ''Serikali imetekeleza ahadi yake ya kulipa madiwani wa halmashauri ambazo mapato yake si makubwa na hazipo daraja A, mishahara yao inalipwa moja kwa moja kutoka Hazina na tayari madiwani wanalipwa shilingi laki tatu na wenyekiti wao wanalipwa laki nne.'' 

Kuhusu akiba ya fedha za kigeni msemaji huyo wa serikali ameeleza kuwa, ''Hivi sasa kwenye akiba yetu ya fedha za kigeni tuna dola za Marekani Bilioni 5.5 hizi zinatuwezesha kununua huduma na bidhaa kwa miezi sita na nusu.''