Saturday , 31st Jul , 2021

Aliyekuwa mshambuliaji wa kati wa klabu ya AS Vita ya DR Congo, Fiston Kalala Mayele ambaye kwasasa amethibitisha kuwa mchezaji mpya wa Yanga, amewatumia salama mashabiki wa klabu hiyo mchana wa leo Julai 31, 2021 kuwataka watulivu na kusubiri mambo mazuri kutoka kwake.

Fiston Kalala Mayele akishangilia moja ya bao alilofunga msimu uliopita 2020-2021 akiwa na uzi wa AS Vita.

Fiston ambaye pia anaichezea timu yake ya taifa ya DR Congo amesema hato kwenye video fupi inayosambaa kwenye mitandano ya kijamii akionekana akiwa kwenye ndege na anayeaminika ni wakala wake safirini kutua nchini Tanzani kumalizana na Wanajangwani hao.

Fiston amesema, "Nawaambia mashabiki wa Yanga bakuwe kimya, timu yetu ya Yanga ina kuwa na ma-objectives mingi kwa hii mwaka, sisi wachezaji tunakuya na furaha, niko mbele na furaha kabisa kucheza timu ya Yanga, me najua tutafanyakazi zetu vile inapenda moyo kufanya, enheee “.

Maneno hayo yaliyotoka moja kwa moja kwenye kinywa cha mchezaji huyo yanathibitisha kuwa jambo lake la kuichezea Yanga kuelekea msimu ujao limekamilika kwa asilimia tisini na kinachosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hiyo ni nyota huyo kuthibitishwa na rasmi.

Fiston alianza kukipiga kwenye klabu ya AS Vita msimu wa mwaka 2019-2020 ambapo alifanikiwa kufunga mabao 7, mabao 5 nyuma ya mfungaji bora wa ligi hiyo, Jackson Muleka aliyekuwa TP Mazembe na sasa anakipiga Standard Liege ya Ubeligiji aliyekuwa na mabao 12.

Msimu huo huo alicheza michezo mitano ya hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa Afrika na kufanikiwa kufunga bao moja pekee sawa na bao alilofunga msimu huu kwenye michuano hiyo baada ya kucheza michezo 5mitano ikiwemo miwili dhidi ya Simba na kutengeneza bao moja.

Kwenye michezo mitano ya mwisho kwa upande wa timu ya taifa, Fiston alifunga bao moja ambalo alilifunga dakika ya 18' Januari 12, 2021 dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha ndani na kuaminika, kinaeleza kuwa ujio wa Fiston umekuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa Ghana, Michael Sarpong ambaye inaelezwa ameachwa na klabu hiyo na amerejea nchini kwao siku ya jana pamoja na Mghana mwenzake, aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho, Lamine Moro.

Wachezaji wengine wakimataifa wanaoripotiwa kuachana na Yanga ni washambuliaji Fiston Abdulazack na Said Ntibazonkiza wote kuyoka Burundi ilhali Carlos Stello (Angola) aliondoka mapema mwezi uliopita na Haruna Niyonzima (Rwanda) aliagwa rasmi kihistoria mchezo mmoja kabla ligi haijamalizika Julai 18, 2021.