Wednesday , 28th Jul , 2021

Mchezaji namba moja Duniani,Novak Djokovic amefuzu kucheza robo Fainali ya michuano ya Olimpiki 2020 baada ya kumshinda Alejandro Davidovich kwa seti za moja kwa moja.

Novak Djokovic(Kushoto) na Kei Nishikori(Kulia) pichani walipokutana kwenye michuano ya US Open mwaka 2014 .

Raia huyo wa Serbia anahitaji ushindi katika hatua tatu zijazo ili afanikiwe kutwaa medali yake ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki baada ya kushinda kwa seti 6-3,6-1.

Upinzani mkubwa kwa Djokovic upo kwa mwenyeji Kei Nishikori ambaye anaendelea kufanya vyema katika mashindano ampao amemshinda Illya Ivashka kwa seti 7-6,6-0.

Nyota hao wataumana katika hatua ya nusu fainali Julai 29 huko Jijini Tokyo nchini Japan wakiwa wanaisaka hatua ya nusu fainali na rekodi inaonyesha wawili hao wameshakutana mara 18 katika mashindano yote, Novak Djokovic ameshinda mara 16 huku Kei Nishikori akishinda mara 2 tu.