Wednesday , 28th Jul , 2021

Msanii Steve RnB amesema yeye ndio mfalme wa muziki wa RnB Bongo na sio Jux wala Ben Pol kwa sababu hawana ujasiri wa kuutaja muziki huo mbele yake na hata jina la 'Steve RnB' alipewa kwa nguvu ya mashabiki.

Kutoka kushoto pichani ni Steve RnB, Jux na Ben Pol

Steve RnB anaendelea kusema hajui kuhusu Jux na Ben Pol japo nao wanatajwa kama ndio wafalme wa muziki huo kwa sababu aina ya RnB wanayoifanya wao ni tofauti na anavyoifanya yeye.

"Kwenye RnB huwezi kutaja bila kuweka jina la Steve hata hao uliowataja hawawezi kuwa na 'courage' kama hiyo kwa kutaja RnB mbele ya majina yao, sijajiita Steve RnB bali mashabiki ndio wamenipa sidhani kama ni vibaya kwa watu kukubali kwamba mimi ndio King wa RnB" amesema Steve RnB

Maelezo zaidi akizungumzia kuhusu ufalme wa muziki wa RnB kati yake, Jux na Ben Pol tazama hapo chini kwenye video.