Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu.
Watu zaidi 74 wamefariki dunia mkoani Ruvuma kwa ajali za bara barani zilizohusisha magari na pikipiki kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mpaka Septemba mwaka huu.
Akizungumza mkuu wa kikosi cha usalama bara barani mkoa wa Ruvuma Selestiani Mtaki amesema vifo hivyo vimetokea baada ya ajali zaidi ya mia tatu na sita kutokea katika maeneo mbali mbali mkoani Ruvuma zilizohusisha vyombo hivyo vya usafiri huku akitaja chanzo kikubwa cha ajali hizo kuwani uzembe wa madereva na hasa waendesha piki piki unaoendelea kuchangia vifo na majeruhi
Amesema jumla ya ajali za bara barani mia tatu na sita ziliripotiwa kutokea katika kipindi hicho na kusababisha vifo ni sirini sanini na nne na majeruhi mia nne kumi na sitana ajali 31 zilitokea bila kusababisha vifo wala majeruhi na lumekuwepo kwa ongezrko la ajali hizo unaochangiwa na ongezeko kubwa la piki piki ambazo zinafikia zaidi mia sita mkoani Ruvuma.
Amesema kufuatia ongezeko hilo la ajali jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiasna na mamlaka nyingine zinaendelea kutoa elimu kwa madereva na waendesha piki piki ambao ndiyo wanaonesha kuwa chanzo kikubwa cha ajali nyingi za bara barani ingawa mutikio wa kupata elimu kwa waendesha piki piki ni mdogo kwa sababu ya ubishi na kutokuonba umuhimu wa kupata mafunzo hayo.
Aidha katika hatua nyingine mkuu wa kikosi cha usalama bara barani amewataka wamiliki na waendesha piki piki mkoani Ruvuma marufu kama boda boda kuwa makini wawapo bara barani pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya alama za bara barani ambazo zimewekwa kwa ajili ya kudhibiti ajali.