Picha ya msanii Chidi Benz na Vanessa Mdee
Chidi Benz ametoa comment yake hiyo kupitia page yake ya Instagram baada ya kumpost Vanessa Mdee kisha kuandika "Sema Tanzania nayo, from no where tumefanya my sister Vannesa Mdee kauchukia muziki, Ilikua tunahitaji sana vitu kutoka sauti ile, sijui wengineo".
Siku za hivi karibuni msanii huyo wa HipHop amekuwa akitoa maoni na mitazamo kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu masuala mbalimbali ya muziki, wasanii na tuzo.