Chanjo ya Corona
Akizungumza Jijini Dodoma Katibu Mkuu, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Afya Prof. Abel Makubi, amesema kuwa kiwanda hicho hakitatengeneza chanjo ya UVIKO tu bali na magonjwa mengine.
"Wataalamu tunao wengi na kiwanda hicho na hakitatengeneza chanjo ya UVIKO-19 pekee, hata ikiisha tutaendelea kuzalisha chanjo nchini" alisema Prof. Makubi.
Aidha, Prof. Makubi amesema serikali haina mpango wa kuwauzia wananchi chanjo ya ugonjwa UVIKO 19 wala kuruhusu mtu yeyote kuingiza chanjo hiyo kinyume na utaratibu utakaowekwa.



