Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Muongozo huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo leo Julai 4, 2021, jijini Dodoma ambapo amesisitiza kuwa mamlaka zihakikishe kuna miundombinu ya maji tiririka, sabuni au vitakasa mikono ili wananchi, wanafunzi, wagonjwa waweze kuvitumia.
''Kwenye ofisi zote za serikali tunashauri watu waende wakiwa wamevaa barakoa na kabla ya kuingia kwenye ofisi hizo na kufanya shughuli ni vyema wanawe mikono'', amesema Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
Aidha Prof. Abel Makubi ameongeza kuwa, ''Miongozo ni ile ile inatakiwa ifuatwe shuleni, vyuoni na taasisi mbalimbali za elimu na Hospitali, kuweka miundombinu inayowezesha kunawa mikono kwa maji tiririka pamoja na kuvaa barokoa muda wote''.
Soma taarifa kamili hapo chini










