Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga
Akizungumza na wandishi wa habari leo Julai Mosi, 2021, Kamanda Onesmo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 15 mwaka huu katika mtaa wa Mji Mpya Jijini Dodoma ambapo alimuuwa kwa kumpiga na jiwe kichwani wakati wakigombea abiria kwenye eneo hilo.
Kamanda Lyanga ameongeza kuwa dereva huyo mara baada ya kuona abiria walianza kugombea na marehemu huku kila mmoja akitaka abiria aingie kwenye gari yake.
Kamanda Lyanga amesema mara baada ya msako kufanyika Juni 19 mwaka huu, wamefanikiwa kumkamata dereva huyo akiwa mafichoni katika Kijiji cha Galapo wilayani Babati mkoa wa Manyara na kusema kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji.
