Monday , 28th Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa kufuatia wimbi la tatu la Corona lililoikumba Dunia kwa takwimu za juzi Tanzania inao wagonjwa takribani 100 wa ugonjwa wa COVID-19.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Juni 28, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini, alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.

"Tanzania tuna wagonjwa wa COVID-19 katika hili wimbi la tatu mpaka taarifa nilizozipata juzi nadhani tuna wagonjwa kama 100 na kati yao si chini ya wagonjwa 70 na wako kwenye matibabu ya gesi na wengine wako kwenye matibabu ya kawaida," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Idadi ya wagonjwa si wengi lakini hatuna budi kujikinga wasiongezeke, hatua tulizozichukua tuliamua kwamba twende na ulimwengu unavyokwenda tuchanje na tuchanje kwa hiari anayetaka achanje asiyetaka atajisikiliza nafsi yake, tumeamua hiyvo kwa sababu Watanzania wengi ambao ni wafanyabiashara wametoka nje ya nchi wamechanja".