Marehemu Mkinga Mkinga amezikwa leo huku mamia ya ndugu, jamaa na marafiki wakielezea pengo aliloliacha na mchango wake katika taaluma yake ya uandishi.
Akimuelezea Marehemu Mkinga, Mwenyekiti wa wazee Chato, Mzee Bigambo Biseko amesema kuwa Mkinga ni mmoja wa tunda la Chato huku akihuzunika kuwa ametangulia mbele za haki ilihali bado walikuwa wanamuhitaji hasa alipojitolea kujenga shule.
Marehemu Mkinga Babu Mkinga alifariki usiku wa kuamkia Juni 24, 2021, katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili MOI, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa, na marehemu ameacha mke na Mtoto mmoja.


