Friday , 5th Dec , 2014

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amewataka wananchi wakiovamia misitu ya hifadhi ya kazimzumbwi wawe wameondoka ifikapo desemba 18 mwaka huu na watakaokaidi, serikali itawaondoa kwa nguvu na kuvunja makazi na nyumba zilizojengwa.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.

Akiongea Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kitaifa wa msitu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema kamwe serikali haiwezi kuendelea kuwavumilia wavamizi hao ambao wamesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ya misitu hiyo ya kazimzumbwi iliyohifadhiwa kisheria tangu mwaka 1954 na

Nyalandu ameongeza kuwa katika operesheni hiyo kubwa itakayofanyika baadae mwezi huu serikaili haitatambua hati au vibali vya watu wanaoishi katika misitu hiyo kwani wanaishi humo kinyume cha sheria na ametaka watu wote humo kuanza kuondoka kwa hiari kabla ya muda huo na amebadilisha hati zote zinazomika na wavamizi hao:

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiongea na washiriki wa mkutano huo Wilayani kisarawe ambao pia wamefanya ziara katika misitu hiyo Kazimzumbwi kujionea uharibifu huo amesema serikali ya mkoa wake imeshapokea maelekezo ya serikali na itatekeleza agizo hilo ambalo litasaidia kuirejesha misitu hiyo katika hali yake kwani kuathirika kwake kumelitia aibu taifa mbele ya jumuiya ya kimataifa ambayo inatambua umuhimu wa misitu ya kazimzumbwi kimazingira na kuboresha hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam:

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na mazingira James Lembeli amesema kamati yake ilishashauri kwamba sheria ilioanzisha misitu hiyo iheshimike ili misitu hiyo iendelee kuwa na manufaa lakini baadhi ya watumishi wa serikali wamesababisha mgogoro mkubwa kati ya wizara ya maliasili na utalii na wizara ya ardhi kuwa wakipima viwanja na kuvigawa kwa wananchi kinyume cha sheria.