Monday , 28th Jun , 2021

Nyota namba moja kwa ubora nchini England katika mchezo wa tenisi, Johanna Konta ameondolewa kwenye michuano mikubwa ya Wimmbledon iliyoanza kutimua vumbi leo kutokana na nyota huyo kuwekwa karantini baada ya kuwa karibu na mgonjwa wa Covid-19.

Mwanamama Johanna Konta akionyesha umwamba wake uwanjani.

Konta alikuwa acheze dhidi ya Katerina Siniakova siku ya Jumanne , anawekwa karantini kwa siku 10 kama ambavyo sheria ya uthibiti wa maradhi hayo zimeainisha huku nafasi yake ikichukuliwa na Yafan Hwan raia wa China .

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 alitarajiwa kufanya vyema kwani msimu uliopita alitinga hadi hatua ya nusu fainali.

Ni pigo jingine kwa mashindano hayo kukosekana kwa mchezaji mwenye hadhi kubwa ambapo wiki iliyopita, Bingwa mtetezi wa mashindano hayo Simona Halep alijiondoa kufuatia kupata majeraha.