Nyota wa Clippers, Khris Middleton akitupia mpira kuisaidia timu yake kupata alama.
Middleton nouma, aibeba Bucks fainali NBAUshindi huo umewafanya Bucks kuongoza kwenye michezo yake miwili mbele ya Hawks wenye ushindi kwenye mchezo mmoja wakitegemea kuendelea kuchuana kuelekea michezo saba ya kuamua hatma ya ubingwa kwenye fainali hiyo.
Middleton amewashangaza wengi kwa kuwambwaga wakali kama vile chipukizi wa Atlanta Hawks, Trae Young na hata nyota mwenzake, Giannis Antetokounmpo.
Kwa upande wa Hawks, wapo njia panda kwani nyota wake Trae Young amepata maumivu ya kifundo cha mguu ambapo watalazimika kusubiri majibu ya MRI ili kubaini ukubwa au udogo wa maumivu hayo.
NBA itaendelea tena saa 10:00 Alfajiri ya kuamkia kesho kwa mchezo mmoja wa mzunguko wa tano wa fainali kwa ukanda wa Mashariki ambapo Los Angeles Clippers watachuana vikali na Phoenix Suns mchezo ambao Suns akishinda atatwaa ubingwa wa ukanda huo.

