Wachezaji wa Italia wakishangilia moja ya magoli yao
Italia wanaungana na Denmark kufuzu baada ya kupata ushindi kwa kumfunga Wales 4-0 katika mechi ya awali, Azzurri wakimsubiri mshindi kati ya Ubelgiji na Ureno watakaocheza jumapili hii uwanja wa Wembley jijini London.
Kufuatia kiwango bora alichokionesha Italia katika michuano hii, ni wazi kwamba timu nyingi zinawahofia kukutana nao , wameshinda mechi zote 4 walizocheza tatu za makundi na 1 ya mtoano katika hatua ya 16 bora.
Kocha Roberto Mancini anajivunia wachezaji bora katika kikosi chake kama Lorenzo Insigne, Nicola Barella, Federico Chiesa, Ciro Immobile, Lorenzo Spinazzola ambaye ametwaa tuzo mara mbili ya mchezaji bora wa mechi.
Italia inarekodi ya kutopoteza michezo 31 mfululizo, imeshinda michezo 26 imesare 5 imefunga magoli 83 imeruhusu kufungwa magoli 8 tu.
Michuano hii ya EURO 2020 inaendelea leo Jumapili hii tarehe 27/6/2021 kwa michezo miwili ambapo Uholanzi dhidi Jamuhuri ya Czech uwanja wa Puskas Hungury, huku mchezo ,mwingine ukiwa ni Ubelgiji dhidi ya Ureno.

