Sunday , 27th Jun , 2021

Jeshi la Magereza nchini linakabiliwa na msongamano wa mahabusu katika magereza mbalimbali mikoani hali inayopelekea mzigo mkubwa kwa wafungwa kulima ili  kuwalisha mahabusu. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo kwenye Gereza la Isanga

Hayo yamebainika leo Julai 27, 2021, wakati wa kikao cha Mahabusu na Wafungwa katika Gereza Isanga na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo, ikiwa ni ziara ya kushughulikia changamoto za mahabusu na wafungwa ili kupunguza msongamano magerezani.

Akisoma taarifa ya Gereza hilo, Mkuu wa Gereza Isanga, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza,Ikobela Fumbuka alitaja idadi ya mahabusu kuwa ni Mia Nne Thelathini na Tisa huku Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Magereza,Keneth Mwambije, akitaja changamoto ya wananchi kuvamia maeneo ya jeshi.