Sunday , 27th Jun , 2021

Hukumu ya Derek Chauvin, afisa wa polisi wa zamani aliyemuua George Floyd kwenye barabara ya Minneapolis mwaka jana, imemuibua Rapper Meek Mill.

Picha ya msanii Meek Mill

Kupitia ukurasa wake wa twitter Meek Mill ameonesha kuunga mkono hukumu hiyo iliyosomwa Ijumaa ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 22 na nusu kwenda Gerezani kwa makosa matatu ikiwa ni pamoja na la mauaji. 

“Kifungo cha miaka 20 jela ni hukumu sahihi kwani kuna marafiki zangu wengi waliwapa hukumu kama hiyo kwa kuuza dawa za kulevya” – ameandika Meek Mill.