Rais wa UEFA Alexander Ceferin
Kamati ya utendaji ya UEFA , imeridhia na kuthibitisha mapendekezo ya kamati ya mashindano kwa upande wa vilabu vya wanaume na vile vya wanawake kuondoa kanuni ya faida ya goli la ugenini.
Rais wa UEFA Alexander Ceferin amesema “kanuni hii imekuwepo tangu mwaka 1965, kwa miaka ya karibuni ilileta mjadala mkubwa sana,kufikia hapa ni sawa tumeshinda vita’’
‘’Tumefanya utafiti na tukajiridhisha kwamba, kwa sasa kanuni hii imepitwa na wakati imefikia mahala inaharibu hadi mbinu za ufundi wakati wa kucheza kwa kuwa timu inayocheza nyumbani inatumia muda mwingi kujihami badala ya kushambulia kwa kuhofia endapo timu ngeni itapata goli basi katika mechi ya mkondo wa pili itawanufaisha wapinzani’’ aliongeza Ceferine
UEFA wamekuwa wakisimamia mashindano yao ngazi ya vilabu kwa upande wa mabingwa Ulaya na ile ya ’ Europa League’pamoja na michuano ya vijana na wanawake, kwa taarifa hii maana yake imefutwa kwa mashindano yote .

