Wednesday , 9th Jun , 2021

Mwimbaji nyota wa muziki wa RnB nchini, Belle 9 ameachia Extended Play (EP) yake ‘Baba Boss Tv’ leo huku kukiwa na collabo kadhaa wa Bongo Fleva kama Young Lunya. 

Picha msanii Belle 9

EP hiyo yenye nyimbo kama ‘Hayatabiliki, ameitoa kama zawadi kwa mwanae wa kwanza Boss, na anaiuza kwa mfumo wa WhatsApp.

“Nimeiita Baba Boss Tv kwasababu leo (tarehe 9, Juni) ndio siku ambayo mtoto wangu wa kwanza (Boss) alizaliwa, kwahiyo naitoa hii kama zawadi na respect kwake kwani kuna kipindi nilisema mimi nilizaliwa tarehe 9 lakini sio kweli” – amesema Belle 9.

Akielezea kwanini Tv msanii huyo amesema kuwa “style na skills nilizozitumia na aina ya muziki unaopatikana kwenye EP hiyo inawezekana kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki ni mtiririko wa muziki ambao inawezekana sio rahisi kuusikia”